Tuambie mtindo unaoutaka — tunakuletea msusi aliyethibitishwa. Lipa kidogo kuthibitisha, na dhamana ya huduma.
Chagua, kisha bonyeza msusi unayemtaka.
Bei kamili · kianzio kidogo kuthibitisha · salio kwa msusi
Kama hali yako ni mojawapo ya hizi — UremboDar inakuondolea usumbufu.
Kukaa salon masaa mengi ni kazi. Msusi anakuja, wewe unapumzika nyumbani.
Huna haja ya kuwaacha wala kutoka nyumbani — tunakuja kwako.
Hakuna foleni, hakuna kusubiri. Booking kwa wakati wako.
Jiandae nyumbani, uwe tayari bila stress ya kusafiri.
Huduma ya hali ya juu, faraghani kwako mwenyewe.
Usitoke nje. Msusi anakuja moja kwa moja kwako.
Bofya msusi unayemtaka na ubonyeze WhatsApp kubuki — sekunde chache.
Tunahakiki upatikanaji na kukutumia bei kamili na kianzio kidogo cha kuthibitisha.
Lipa kianzio kuthibitisha (na dhamana). Salio unamlipa msusi akimaliza.
Bofya mtindo — tunakuunganisha na msusi anayekuja nyumbani.
Ukibuki kupitia UremboDar, huduma ina dhamana. Hajafika au hujaridhika — tunakuletea msusi mwingine bila malipo ya ziada. Salama, safi, kwa wakati.
"Nilisuka box braids nyumbani Jumamosi bila kupoteza siku nzima salon. Msusi professional kabisa."
"Knotless zangu zilikuja nyumbani kwa wakati, safi sana. Sikuamini ni rahisi hivi!"
"Kila mwezi nasuka kupitia UremboDar — booking dakika moja na wanakuja. Bora kuliko salon."
Jiunge na UremboDar bila malipo. Tunakuletea wateja waliothibitisha booking — wewe unasuka tu. Hakuna ada za kuanza, unapata bei yako kamili.
Jiunge kama Msusi →Kuweka booking ni bure. Bei inayoonyeshwa ni kamili. Unalipa kianzio kidogo kuthibitisha booking, na salio unamlipa msusi mwenyewe akimaliza huduma.
Inategemea msusi. Tutakuambia wazi kabla ya kuthibitisha kama nywele zimejumuishwa au unazileta mwenyewe.
Kila msusi anapigiwa simu binafsi, tunahakiki kitambulisho, ujuzi na kazi zake za nyuma kabla ya kuwekwa kwenye jukwaa.
Tunakupanga msusi mwingine bila malipo ya ziada. Hiyo ndiyo dhamana yetu.
Kwa sasa Dar es Salaam — Masaki, Oyster Bay, Mikocheni, Mbezi Beach, Kinondoni, Upanga na zaidi.